SERIKALI ITAENDELEA KUWALINDA WENYE VIWANDA-MAJALIWA.

19 Septemba, 2021 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuwalinda wenye viwanda nchini na haitavumilia kuona wawekezaji wakinyanyaswa. Pia, Waziri Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Samia amewaagiza wasaidizi wake  wasimamie mwenendo mzima wa masoko ya mazao mbalimbali nchini likiwemo na zao la Kahawa ili kuhakikisha wakulima wananufaika